Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mussa Azzan Zungu, akisalimiana na Spika wa Bunge la Uingereza (House of Commons), Sir Lindsay Hoyle, wakati wa kikao cha Baraza la Uongozi la Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), kilichofanyika katika moja ya ukumbi kwenye Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha (AICC), leo Oktoba 6, 2026.
Spika Zungu aliambatana na Wawakilishi wa Bunge la Tanzania katika Mkutano wa 153 wa IPU unaofanyika Arusha kuanzia Oktoba 5 hadi 9, 2026 ukiwakutanisha viongozi wa mabunge, wabunge na wawakilishi kutoka nchi 184 duniani. #IPU153Tanzania
