Spika wa Bunge la Maldives, Abdul Raheem Abdulla, ni miongoni mwa wageni waliotembelea Banda la “Karibu Tanzania” katika Mkutano wa 153 wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), unaofanyika jijini Arusha.
Akiwa katika banda hilo, Abdulla amepata fursa ya kufahamu safari ya Tanzania katika demokrasia na maendeleo, huku akieleza kufurahishwa na hatua iliyofikiwa katika utekelezaji wa miradi mikubwa ya kimkakati, ikiwemo Reli ya Kisasa (SGR), Bwawa la Julius Nyerere, Daraja la Busisi (Magufuli), uendelezaji wa Bandari ya Dar es Salaam, pamoja na miundombinu inayoandaliwa kwa ajili ya Mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2027.
#IPU153Tanzania
