Tanzania imeelezwa kuwa miongoni mwa nchi za Afrika zinazopiga hatua katika kuimarisha afya ya mama na mtoto, huku uzoefu wake ukitajwa kuwa muhimu katika kuharakisha utekelezaji wa ajenda ya Umoja wa Afrika (AU) ya “Sifuri Tatu.”
Ajenda hiyo inalenga kuhakikisha hakuna mwanamke anayejifungulia nyumbani, hakuna vifo vinavyoweza kuzuilika vya mama na mtoto, na hakuna mtoto anayekosa chanjo.
Hatua za Tanzania katika eneo hilo zimejadiliwa na viongozi wa mabunge na wataalamu wa afya katika Mkutano wa Afya ya Mama na Mtoto Afrika, uliofanyika pembezoni mwa Mkutano wa 153 wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) jijini Arusha.
Mkutano huo umeweka Tanzania katika nafasi ya kushirikisha uzoefu wake na nchi nyingine za Afrika katika kuimarisha huduma za afya ya mama, mtoto mchanga na mtoto.
#IPU153Tanzania
