You are currently viewing RAIS MPYA WA IPU NI SPIKA WA BUNGE LA AUSTRALIA

RAIS MPYA WA IPU NI SPIKA WA BUNGE LA AUSTRALIA

Spika wa Bunge la Australia, Milton Dick, ameshinda urais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), akimrithi Dk Tulia Ackson, aliyeongoza kwa miaka mitatu tangu 2023.

Dick, ameshinda nafasi hiyo kwa kupata kura 182 sawa na asilimia 56, akiwashinda Seneta Rojo Edwards Silva wa Chile aliyepata kura sita na Sahiba Gafarova wa Azerbaijan kura 124.

Uchaguzi huo, umefanyika leo Oktoba 9, 2026 ikiwa ni siku ya mwisho ya Mkutano wa 153 wa Umoja wa IPU, uliofanyika Arusha.

Kwa matokeo hayo, Dick anakuwa Rais wa 32 wa IPU, huku wadhifa wa Dk Tulia wa Tanzania ukifika mwisho rasmi.

#IPU153Tanzania

Leave a Reply