You are currently viewing RAIS SAMIA: TANZANIA INAJIVUNIA KUWA MWENYEJI MKUTANO WA IPU

RAIS SAMIA: TANZANIA INAJIVUNIA KUWA MWENYEJI MKUTANO WA IPU

Rais Samia Suluhu Hassan, amesema Serikali ya Tanzania inajivunia kupewa nafasi ya kuwa mwenyeji wa Mkutano wa 153 wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU).

Mkuu huyo wa nchi, ameyasema hayo leo, Oktoba 5, 2026 katika ujumbe wake kwa washiriki wa mkutano wa IPU unaofanyika Arusha kuanzia Oktoba 5 hadi 7, mwaka huu.

Amesema hatua ya Tanzania kuwa mwenyeji wa mkutano huo, inaimarisha utendaji wa Serikali na kuongeza uwajibikaji kwa wananchi.

“Serikali yangu inalitazama jukumu hilo kwa umuhimu mkubwa, ikitambua kwamba nafasi ya Bunge inaongeza nguvu katika kazi ya Serikali na katika uwajibikaji tunaodaiwa kwa wananchi wa Tanzania,” amesema.#IPU153Tanzania

Leave a Reply