Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mwigulu Nchemba, akishiriki Mkutano wa 153 wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, leo Oktoba 5, 2026, katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha (AICC), jijini Arusha.
Mkutano huo umeanza leo Oktoba 5 hadi 9, 2026, jijini Arusha, ukiwakutanisha wajumbe kutoka mabunge ya mataifa 183 na washiriki zaidi ya 2000 kutoka maeneo mbalimbali duniani.#IPU153Tanzania
